النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ ۖ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتٌۢ بِأَمْرِهِۦٓ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ١٢
{12} Yaani, aliwatiishia vitu hivi kwa manufaa yenu na aina mbalimbali za masilahi yenu, kiasi kwamba hamuwezi kukosa kuzihitaji abadan. Kwa maana, usiku mnakaa humo, na kulala, na kupumzika. Na mchana mnaenea katika maisha yenu na manufaa ya dini yenu na dunia yenu. Na kutokana na jua na mwezi mnapata mwangaza na mng'ao, na kuifanya miti kuwa vizuri, na matunda, na mimea, na kukausha unyevu, na kuondoa baridi yenye madhara kwa dunia na miili na mahitaji mengine ya lazima na ya kawaida yanayotegemea kuwepo kwa jua na mwezi. Na pia ndani ya hivyo na katika nyota kuna mapambo kwa mbingu na mwongozo katika giza la nchi kavu na baharini na kujua nyakati na kuhesabu nyakati. Hivyo vyote kuna ushahidi na ishara mbalimbali, na ndiyo maana akavikusanya katika kauli yake, "Hakika katika hayo zipo ishara kwa kaumu watumiao akili." Yaani, wale ambao wana akili ambazo wanazitumia katika kuzingatia na kutafakari kile kilichoandaliwa kwa ajili yake. Zinafahamu kile kinachokiona na kukisikia, na si kama kuona kwa wale walioghafilika ambazo fungu lao katika kuangalia ni kama fungu la wanyama ambao hawana akili.