انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١٥

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ ٱلْمَيْتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحْمَ ٱلْخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيْرِ ٱللَّهِ بِهِۦ ۖ فَمَنِ ٱضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ١١٥

{115} "Amewaharimishia." Vitu vinavyoleta madhara vimeharamishwa kwenu, navyo ni kama vile mzoga,hapa ni pamoja na kila kilichokufa kwa njia isiyo ya sahihi kisheria, isipokuwa mzoga wa nzige na samaki ambavyo vimeruhusiwa. "Na damu" iliyomwagika, Ama kwa ile inayobaki katika mishipa na nyama, haidhuru. "Na nyama ya nguruwe" kwa uchafu wake na ubaya wake, na hii inajumuisha nyama yake, mafuta yake, na sehemu zake zote. "Na mnyama aliyechinjwa kwa ajili isiyokuwa ya Mwenyezi Mungu;" kama vile anayechinja kwa ajili ya masanamu, makaburi na kadhalika, kwa sababu lengo lake ni shirki. "Lakini anayelazimishwa bila ya kuasi" kwa kitu chochote kutokana na vilivyoharimishwa; wakati kuna haja halisi na mtu anaogopa kuangamia kama hatakula, basi hana dhambi ikiwa si mwenye uadui na wala si muasi. Yaani, ikiwa hana nia ya kula kitu kilichoharamishwa, na hawezi kupata chakula halali au amezidisha kiasi cha mahitaji ya lazima. Hii ndiyo ambayo ameharamisha Mwenyezi Mungu kati ya mubaah.