انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١١٢–١١٣

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ ءَامِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ ٱللَّهِ فَأَذَٰقَهَا ٱللَّهُ لِبَاسَ ٱلْجُوعِ وَٱلْخَوْفِ بِمَا كَانُوا۟ يَصْنَعُونَ ١١٢ وَلَقَدْ جَآءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْهُمْ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ ٱلْعَذَابُ وَهُمْ ظَـٰلِمُونَ ١١٣

{112 - 113} Mji huu ni Makka tukufu, ambayo ilikuwa na amani, na utulivu, ambamo hakuna yeyote aliyefadhaishwa. Na watu wa kipindi cha Jahiliyya walikuwa wakiuheshimu, kiasi kwamba mmoja wao angemkuta mtu aliyemuua baba yake na kaka yake, lakini hangeweza kumfadhaisha pamoja na ukali wa hasira zao na majivuno ya Kiarabu. Kwa hivyo kukawa humo na amani kamili ambayo haikutokea kwa miji mingineyo. Na vile vile kulikuwa na riziki kunjufu. Ulikuwa mji ambapo hakukuwa na mimea wala miti, lakini Mwenyezi Mungu akaurahisishia riziki ambayo ilikuwa akiujia kutokea kila mahali. Kisha wakajiwa na Mtume kutoka miongoni mwao ambaye walijua uaminifu wake na ukweli wake. Akawalingania kwenye mambo kamilifu zaidi, na akawakataza mambo mabaya, lakini wakamkadhibisha na wakakufuru neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yao, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akawaonjesha kinyume cha walichokuwa ndani yake, na akawavisha "vazi la njaa" ambayo ni kinyume cha utele, "na hofu" ambayo ni kinyume cha amani. Na hayo ni kwa sababu ya matendo yao, ukafiri wao, na kutoshukuru kwao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu wenyewe.