انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ابراهيم
السورة ١٤

ابراهيم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٢

هَـٰذَا بَلَـٰغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا۟ بِهِۦ وَلِيَعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَـٰبِ ٥٢

{52} Alipobainisha ubainisho ulio wazi katika Qur-ani hii, akasema katika kuisifu, "Huu ni ufikishaji kwa watu." Yaani, ili wafike kwayo, na ili wachukue masurufu ya kuwafikisha katika nafasi za juu zaidi na matukufu yaliyo bora zaidi. Kwa sababu ya kile ilichojumuisha cha misingi, matawi na elimu zote wanazozihitaji waja, “Na ili waonywe kwao” kwa sababu ya vitishio vilivyomo ndani yake dhidi ya kutenda matendo maovu na yale ambayo Mwenyezi Mungu amewaandalia watu wake ya adhabu. “Na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja" ambapo ameweka humo ushahidi na hoja mbalimbali juu ya uungu wake na upweke wake, basi yakawa hayo ni haki ya yakini. "Na wapate kukumbuka wenye akili." Yaani, waweze kukumbuka wenye akili kamili yale yenye kuwafaa kwa hivyo wakayafanya, na yenye kuwadhuru, kwa hivyo wakayaacha. Na kwa hayo ndiyo wakawa wenye akili na ufahamu. Kwa sababu kupitia katika Qur-ani, yalizidi maarifa yao na rai zao na fikira zao yakatiwa nuru walipoichukua katika hali yake ya upya na laini. Kwa maana hiyo hailinganii isipokuwa kwa maadili na matendo ya hali ya juu na bora zaidi, na haya hayaonyeshwi isipokuwa kwa ushahidi wenye nguvu zaidi na wa wazi zaidi. Na kanuni hii, ikiwa mja mwerevu atajifunza, daima hataacha kuendelea kuinuka juu na kupanda katika kila sifa njema. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Imekamilika tafsiri ya Surat Ibrahim, mwandani wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani ziwe juu yake.