انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · ابراهيم
السورة ١٤

ابراهيم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٧

يُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱلْقَوْلِ ٱلثَّابِتِ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلظَّـٰلِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ ٢٧

{27} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba Yeye huwaimarisha waja wake waumini ambao walifanya wajibu wa kuamini kimoyo kikamilifu ulio juu yao, ambako kunalazimu kuwepo kwa matendo ya viungo nako kweli kuvizalisha. Na Mwenyezi Mungu huwaimarisha katika uhai wa dunia wanapotokewa na fikira potofu kwa kuwaongoa kufikia yakini, na wanapotokewa na matamanio kwa kuwapa utashi thabiti wa kuupendelea kile anachokipenda Mwenyezi Mungu juu ya matamanio ya nafsi na utashi wake. Na katika akhera wakati wa kufa kwa kuwaimarisha juu ya dini ya Kiislamu na mwisho mwema. Na kaburini wakati Malaika wale wawili watakapowauliza kwa kuwapa jibu sahihi, maiti atakapoambiwa: Ni nani Mola wako Mlezi? Na Dini yako ni ipi? Na Nabii wako ni nani? Yeye Mwenyezi Mungu atawaongoa kufikia jawabu sahihi kwa kusema: Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, na Uislamu ndiyo dini yangu, na Muhammad ndiye Nabii wangu. "Na Mwenyezi Mungu huwapoteza madhalimu" wasifikie usahihi katika dunia na Akhera, na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali walizidhulumu wenyewe nafsi zao. Aya hii inaashiria majaribio, adhabu, na raha ya kaburini, kama ilivyokuja kuhusiana na hayo katika maandiko mengi matakatifu kutoka kwa Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake – kuhusu majaribio ya kaburini, na maelezo yake, na starehe zake na adhabu yake.