يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَلَمَّآ أَن جَآءَ ٱلْبَشِيرُ أَلْقَىٰهُ عَلَىٰ وَجْهِهِۦ فَٱرْتَدَّ بَصِيرًا ۖ قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّىٓ أَعْلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ ٩٦
{96} "Basi alipofika tu mbashiri huyo” kwa bishara ya ukaribu wa kukutana na Yusuf, na ndugu zake, na baba yao, “akalitupa” yaani, shati hilo “usoni pake, basi akarejea kuona.” Yaani, alirudi katika hali yake ya awali ya kuona baada ya macho yake kuwa meupe kwa sababu ya huzuni, kisha akawaambia wale waliokuwa karibu naye miongoni mwa watoto wake na ahali zake ambao walikuwa wakiifanyia masihara rai yake na wakistaajabu naye, huku akiwa amewashinda juu yao na akijivunia neema ya Mwenyezi Mungu juu yake: “Sikuwaambia kuwa mimi ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua nyinyi?” Kwa kuwa nilikuwa ninatarajia kukutana na Yusuf, nikingoja kwisha kwa wasiwasi yangu kubwa, na msiba wangu, na huzuni.