انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨٩

قَالَ هَلْ عَلِمْتُم مَّا فَعَلْتُم بِيُوسُفَ وَأَخِيهِ إِذْ أَنتُمْ جَـٰهِلُونَ ٨٩

{89} Na jambo hilo lilipokwisha na kufikia kilele chake, Yusuf akafanya huruma mkubwa sana kwao, na akajitambulisha kwao na akawalaumu, akasema: "Je, mnajua yale mliyomfanyia Yusuf na nduguye?” Ama Yusuf, basi ni dhahiri mno kile walichomfanyia, na ama nduguye, basi landa huenda - na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi – ni kauli yao, " Akiwa ameiba huyu, basi hakika nduguye vile vile aliiba hapo zamani.” Au ni kwamba sababu iliyomtenganisha yeye na baba yake wao ndio walikuwa sababu yake na msingi uliosababisha hilo "mlipokuwa wajinga?” Na hii ni aina fulani ya udhuru aliowakubalia kwa sababu ya ujinga wao au karipio kwao kwa kuwa walifanya kitendo cha wajinga, pamoja na kwamba hakiwafaili wala hakiendani nao.