يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَأْتِيَنِى بِهِمْ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْحَكِيمُ ٨٣
{83}. Basi waliporudi kwa baba yao na kumwambia habari hii, huzuni yake ikazidi na dhiki yake ikaongezeka maradufu, na akawatuhumu tena katika suala hili kama alivyowatuhumu katika lile la kwanza, na "Akasema: Bali nafsi zenu zimewashawishi kwenye jambo fulani. Basi subira ni nzuri!” Yaani, ninakimbilia juu ya hayo kwenye subira nzuri ambayo haiambatani na hasira, wala kupapatika, wala kuwalalamikia viumbe. Kisha akakimbilia katika kutafuta faraja wakati alipoona kwamba jambo hilo limekuwa kali sana na dhiki yake imekuwa mbaya zaidi, kwa hivyo akasema: "Huenda Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja.” Yaani, Yusuf, Binyamin, na yule ndugu yao mkubwa ambaye aliamua kukaa Misri. "Hakika Yeye ndiye Mwenye kujua vyema” ambaye anaijua hali yangu na haja yangu ya faraja yake na neema yake na dharura yangu juu ya ihsan yake "Mwenye hekima." Ambaye alikiwekea kila kitu kipimo, na akaliwekea kila jambo mwisho wake kulingana na kile hekima Yake ya kiungu inahitaji.