انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٥

قَالَ ٱجْعَلْنِى عَلَىٰ خَزَآئِنِ ٱلْأَرْضِ ۖ إِنِّى حَفِيظٌ عَلِيمٌ ٥٥

{55} Basi Yusuf akasema, akitafuta masilahi ya uma, “Nifanye msimamizi wa hazina za nchi;” yaani, hazina za mazao ya nchi na mavuno yake, kama mwakilishi, mlinzi na mwendeshaji. "Kwani hakika mimi ni mlinzi mzuri, mwenye elimu sana.” Yaani, mlinzi kwa yale ninayosimamia. Hakuna kinachoweza kupotea kwayo kwa kuyaweka mahali pasipokuwa pake. Na ninadhibitii vinavyoingia na vinavyotoka nje. Ninajua vyema jinsi ya kuviendesha, na kutoa, kuzuia, na kutenda vyema katika aina zote za utendaji. Na hili halikuwa kuwania kukubwa kwa Yusuf juu ya uongozi. Bali ni utashi wake tu kufikisha manufaa kwa umma. Na alijijua mwenyewe kuna anatosha hilo, na kwamba ni muaminifu, na kuhifadhi kiasi ambacho wao hawakuwa wanajua. Basi ndiyo maana, akamwomba mfalme ampe usimamizi wa hazina za nchi, kwa hivyo mfalme akamfanya kuwa msimamizi wa hazina za nchi.