انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣٧

قَالَ لَا يَأْتِيكُمَا طَعَامٌ تُرْزَقَانِهِۦٓ إِلَّا نَبَّأْتُكُمَا بِتَأْوِيلِهِۦ قَبْلَ أَن يَأْتِيَكُمَا ۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِى رَبِّىٓ ۚ إِنِّى تَرَكْتُ مِلَّةَ قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَهُم بِٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ كَـٰفِرُونَ ٣٧

{37} Kwa hivyo, "Akasema" akiwaitikia maombi yao: "Hakitawajia chakula mtakachoruzukiwa isipokuwa nitawaambia hakika yake kabla ya kuwajia." Yaani, basi mioyo yenu na itulie kwa maana nitaharakisha kufasiri ndoto zenu, na chakula chenu cha mchana au cha jioni jambo la kwanza kitakapowajia, isipokuwa nitakuwa nimewaambia hakika yake kabla ya kuwajia. Na huenda Yusuf, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alikusudia kuwalingania kwenye imani katika hali hii ambayo ndani yake ilionekana haja yao, ili wito wake uwe wa kuwaathiri zaidi wa kukubaliwa zaidi nao. Kisha akasema, "Hayo" niliyowafasiria "ni katika yale aliyonifundisha Mola wangu Mlezi." Yaani, hii ni katika elimu ya Mwenyezi Mungu aliyonifundisha na akanifanyia wema kwayo. Na hayo ni kwamba, "Hakika mimi nimeacha mila ya kaumu wasiomwamini Mwenyezi Mungu, na wakawa wameikufuru Akhera." Na kuacha, kama kunavyokuwa kwa yule aliyeingia katika kitu kisha akakihama, pia kunakuwa kwa yule ambaye hakuingia humo hata kidogo. Kwa hivyo, haiwezi kusemwa kwamba Yusuf hapo awali alikuwa wa mila isiyokuwa ya Ibrahim.