انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٣

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ ٱلْقَصَصِ بِمَآ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِۦ لَمِنَ ٱلْغَـٰفِلِينَ ٣

{3} "Sisi tunasimulia simulizi nzuri zaidi." Na hilo ni kwa sababu ya ukweli wake, usahili wa maneno yake, na umaridadi wa maana zake, "kwa kukufunulia Qur-ani hii." Yaani, kwa sababu ya yale yaliyomo ndani ya Qur’ani hii ambayo tulikufunulia wewe na tukakufadhilisha wewe kwayo juu ya Mitume wengine wote. Na hiyo ni neema tupu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ihsan. "Na ijapokuwa kabla ya haya ulikuwa miongoni mwa walioghafilika." Yaani, hukuwa unajua ni nini Kitabu wala imani kabla ya Mwenyezi Mungu kukufunulia wahyi, lakini tumekifanya kuwa ni nuru ambayo kwayo tunamwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na alipozisifu hadithi zilizomo ndani ya Qur-ani hii na kwamba ni hadithi nzuri kabisa, na hakuna hadithi katika kitabu chochote kama zilizomo katika Qur-ani hii, akataja kisa cha Yusuf, na baba yake, na ndugu zake, hadithi ya ajabu na nzuri, kwa hivyo akasema: