انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يوسف
السورة ١٢

يوسف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٥

وَٱسْتَبَقَا ٱلْبَابَ وَقَدَّتْ قَمِيصَهُۥ مِن دُبُرٍ وَأَلْفَيَا سَيِّدَهَا لَدَا ٱلْبَابِ ۚ قَالَتْ مَا جَزَآءُ مَنْ أَرَادَ بِأَهْلِكَ سُوٓءًا إِلَّآ أَن يُسْجَنَ أَوْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ٢٥

{25} Alipokataa kuitikia ombi lake baada ya kumshawishi kukubwa, akaenda ili amtoroke na aharakishe kutoka nje ya mlango ili ajinasue na ayatoroke majaribu hayo, lakini mwanamke huyo akamtangulia kwenda huko, na akaishikilia nguo yake, kwa hivyo akalirarua shati lake. Na walipofika mlangoni katika hali hiyo, wakamkuta bwana wake - yaani, mumewe - hapo mlangoni, na akaona jambo linalomsumbua sana, kwa hivyo mwanamke huyo akaharakisha kusema uongo, na kwamba kushawishi huko kulitoka kwa Yusuf. Akasema: "Hakuna malipo ya mwenye kutaka kumfanyia mabaya mkeo" wala hakusema: aliyemfanyia ubaya mkeo, kwa ajili ya kujitoa katika hatia na kumtoa Yusuf pia katika hatia ya kufanya kitendo hicho, lakini mzozo huo ulikuwa tu katika utashi na kushawishi; "isipokuwa afungwe au kupewa adhabu chungu." Yaani, au aadhibiwe adhabu chungu.