يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ذَٰلِكَ مِنْ أَنۢبَآءِ ٱلْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۖ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ أَجْمَعُوٓا۟ أَمْرَهُمْ وَهُمْ يَمْكُرُونَ ١٠٢
{102} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomsimulia kisa hiki Muhammad – rehema na amani ya Mwenyezi Mungu zimfikie - Mwenyezi Mungu akamwambia: "Hizo" [Habari] ambazo tulikujulisha juu yake "ni katika habari za ghaibu” ambazo lau kuwa si sisi kukufunulia, basi hazingekufikia habari hizi kubwa. Kwa maana hukuwepo "pamoja nao walipoazimia jambo lao hilo;” yaani, wale ndugu zake Yusuf, "walipokuwa wanafanya njama zao” dhidi yake wakati walipofungiana ahadi kumtenganisha na baba yake katika hali ambayo hakuna awezaye kuijua isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wala hawezi yeyote kuijua isipokuwa kwa kuelimishwa na Mwenyezi Mungu juu yake. Kama Yeye Mtukufu alivyosema aliposimulia kisa cha Musa na yaliyompata, akataja hali ambayo viumbe hawawezi kufikia kujua isipokuwa kwa wahyi wake, kwa hivyo akasema, “Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipompa Musa amri, wala hukuwa katika waliohudhuria.” Mpaka mwisho wa Aya hii. Basi huu ndio ushahidi wa wazi kabisa kwamba mwenye kuzileta ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa uhakika.