يوسف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ لَا تَقْتُلُوا۟ يُوسُفَ وَأَلْقُوهُ فِى غَيَـٰبَتِ ٱلْجُبِّ يَلْتَقِطْهُ بَعْضُ ٱلسَّيَّارَةِ إِن كُنتُمْ فَـٰعِلِينَ ١٠
{10} Yaani, "Akasema msemaji" miongoni mwa ndugu zake Yusuf ambao walitaka kumuua au kumfukuzia mbali "Msimuuwe Yusuf" kwa maana kumuua ni dhambi kubwa na mbaya zaidi. Lakini yanayokusudiwa yanaweza patikana kwa kumpeleka mbali na baba yake bila ya kumuua, lakini fikieni jambo la kumweka mbali kwa kumtumbukiza "ndani ya kisima" na mumtishie kwamba asijulishe yeyote juu yenu, bali aseme kuwa yeye ni mtumwa anayemilikiwa, aliyetoroka [kwenu] ili aokotwe na "baadhi ya wasafiri" ambao wanasafiri kwenda sehemu za mbali ili wamhifadhi pamoja nao. Na mzungumzaji huyu ndiye wa maoni bora zaidi kati yao kuhusiana na Yusuf na mwema wao zaidi na mchamungu wao zaidi katika suala hili. Kwa maana, baadhi ya uovu ni mdogo zaidi kuliko baadhi yake na madhara mepesi huepukwa kwayo madhara makubwa; basi walipokubaliana juu ya maoni haya: