هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَالَ يَـٰقَوْمِ أَرَءَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّى وَرَزَقَنِى مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَمَآ أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَآ أَنْهَىٰكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا ٱلْإِصْلَـٰحَ مَا ٱسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا تَوْفِيقِىٓ إِلَّا بِٱللَّهِ ۚ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ ٨٨
{88} Shuaibu "akasema" akiwaambia, "Enyi kaumu yangu! Mwaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi?" Yaani, yakini na utulivu juu ya usahihi wa yale niliyokuja nayo, "na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake?" Yaani, Mwenyezi Mungu amenipa sampuli za mali alizonipa, "Na" mimi sitaki "kuwahalifu nikafanya yale ninayowakataza." Sitaki kuwakataza kupunja katika vipimo na mizani, kisha mimi mwenyewe ninaifanya hayo mpaka nikawa ninalaumiwa katika hilo. Bali mimi siwakatazi jambo lolote isipokuwa mimi ndiye mtu wa kwanza kuliacha. "Sitaki isipokuwa kutengeneza kiasi ninavyoweza;" yaani, sina malengo zaidi ya kwamba zitengenee hali zenu na yanyooke manufaa yenu, wala sina malengo yoyote ambayo ni mahususi kwangu peke yangu kwa kulingana na uwezo wangu. Na kwa kuwa hili lina aina fulani ya kujitakasa nafsi, akalizuia hili kwa kauli yake: "Na sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Mwenyezi Mungu " Yaani, sipati kuwezeshwa kufanya heri na kujiepusha na maovu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kwa uwezo wangu wala kwa nguvu yangu. "Kwake Yeye ninategemea;" yaani, nimemtegemea katika mambo yangu na nina imani kwamba atanitosheleza. "Na kwake Yeye ninarudi" katika kutekeleza yale aliyoniamrisha miongoni mwa aina mbalimbali za ibada, na katika kujiweka karibu huku naye kwa vitendo vya heri vyote, na kwa mambo haya mawili ndiyo hali za mja zinanyooka, ambayo ni kutafuta msaada kutoka kwa Mola wake Mlezi na kurejea kwake. Kama alivyosema yeye Mtukufu: "Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye." Na akasema: “Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.”