انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · هود
السورة ١١

هود

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨١

قَالُوا۟ يَـٰلُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوٓا۟ إِلَيْكَ ۖ فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ ٱلَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ إِلَّا ٱمْرَأَتَكَ ۖ إِنَّهُۥ مُصِيبُهَا مَآ أَصَابَهُمْ ۚ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ ٱلصُّبْحُ ۚ أَلَيْسَ ٱلصُّبْحُ بِقَرِيبٍ ٨١

{81} Na kwa sababu ya hayo, jambo lake lilipofika mwisho wake na dhiki ikawa kubwa zaidi; "Wakamwambia: Hakika Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi." Yaani wakamwambia hali yao ili moyo wake utulie. "Hawa hawatakufikia" kwa madhara. Kisha Jibril akafanya kwa bawa lake, na akayapofua macho yao, kwa hivyo wakaondoka kwenda wakimtishia Luti kwamba warudi alfajiri. Na Malaika hao wakamuamuru Lut'i kwamba asafiri na ahali zake "usiku ungalipo" kabla ya mapambazuko Ili waweze kuwa mbali na kijiji chao. "Wala yeyote miongoni mwenu asitazame nyuma;" yaani, harakisheni kutoka, na iwe hamu yenu ni kuokoka, wala msigeuke kuyaangalia yale yaliyo nyuma yenu, "isipokuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba utakaowafika hao." Kwa sababu, yeye anashiriki katika dhambi hiyo na kaumu yake, kwa hivyo alikuwa akiwaonyesha kaumu yake wageni wa Luti wanapomjia wageni. "Hakika miadi yao ni asubuhi" na ni kana kwamba Luti alitaka hilo lifanyike kwa haraka, basi akaambiwa: "Je, asubuhi si karibu?"