هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَتِلْكَ عَادٌ ۖ جَحَدُوا۟ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا۟ رُسُلَهُۥ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ ٥٩
59. "Na hao ndio kina 'Aadi" ambao Mwenyezi Mungu aliwafikishia yale aliyowafikishia kwa sababu ya dhuluma yao, kwa sababu "Walizikufuru Ishara za Mola wao Mlezi." Na ndiyo maana wakamwambia Hud: Hukutujia na ushahidi wowote ulio wazi! Kwa hivyo, ikabainika kwa hili kuwa wao walikuwa na yakini juu ya ulinganizi wake, lakini walikaidi tu na wakakataa, "na wakawaasi Mitume wake." Kwa sababu, mwenye kumuasi Mtume mmoja, basi hakika ameshawaasi Mitume wote; kwa sababu, wito wao ni mmoja. "Na wakafuata amri ya kila jabari;" yaani, anayejipa mamlaka juu ya waja wa Mwenyezi Mungu kwa kuwakandamiza. "Mkaidi;" yaani, anayezikaidi ishara za Mwenyezi Mungu, na wakamuasi kila mshauri na mwenye kuwahurumia vikubwa, na wakamfuata kila mwenye kuwadanganya anayetaka kuwaangamiza. Basi hakuna shaka kwamba ndiyo sababu ya Mwenyezi Mungu kuwaangamiza.