هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنِّى تَوَكَّلْتُ عَلَى ٱللَّهِ رَبِّى وَرَبِّكُم ۚ مَّا مِن دَآبَّةٍ إِلَّا هُوَ ءَاخِذٌۢ بِنَاصِيَتِهَآ ۚ إِنَّ رَبِّى عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ ٥٦
{56} "Hakika mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu." Yaani, nimemtegemea Mwenyezi Mungu katika mambo yangu yote, "Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi." Yaani, Yeye ndiye Muumba wa kila kitu, na mwendeshaji wetu na nyinyi, naye ndiye aliyetulea. "Hakuna kiumbe yeyote isipokuwa Yeye anamwendesha atakavyo," basi hutafanya harakati zozote wala kutulia isipokuwa kwa idhini yake. Kwa hivyo, ikiwa mtakusanyika nyote pamoja ili kunishambulia, na Mwenyezi Mungu hakuwapa mamlaka dhidi yangu, basi hamtaweza hilo. lakini akiwapa mamlaka dhidi yangu, basi ni kwa sababu ya hekima aliyotaka. "Hakika Mola wangu Mlezi yuko kwenye njia iliyonyooka." Yaani, Yeye yuko kwenye uadilifu, na haki, na ni Mwenye hekima, na Mwenye kusifiwa katika hukumu zake na majaliwa Yake, na [katika] sheria yake na amri yake, na katika malipo Yake, na thawabu zake na adhabu yake. Vitendo vyake havitoki katika njia iliyonyooka ambayo anahimidiwa na kusifiwa kwayo.