هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
تِلْكَ مِنْ أَنۢبَآءِ ٱلْغَيْبِ نُوحِيهَآ إِلَيْكَ ۖ مَا كُنتَ تَعْلَمُهَآ أَنتَ وَلَا قَوْمُكَ مِن قَبْلِ هَـٰذَا ۖ فَٱصْبِرْ ۖ إِنَّ ٱلْعَـٰقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ ٤٩
{49} Mwenyezi Mungu akamwambia Nabii wake Muhammad -rehema na Amani za Mwenyezi Mungu zimshukie - baada ya kumsimulia kisa hiki kilichoelezwa kwa kina, ambacho hakuna akijuaye isipokuwa yule aliyemneemesha kwa ujumbe wake: "Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala kaumu yako, kabla ya haya" ndiyo wakasema kwamba: Hakika alikuwa alikiyajua. Basi sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, na mshukuru, na subiri katika yale uliyo juu yake ya Dini iliyonyooka, na njia iliyonyooka, na kulingania kwa Mwenyezi Mungu. "Hakika Mwisho ni wa wachamungu" ambao wanajiepusha na ushirikina na maasi mengine yote, basi mwisho utakuwa wako dhidi ya kaumu yako kama ulivyokuwa wa Nuhu dhidi ya kaumu yake.