هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَمْرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ قُلْنَا ٱحْمِلْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ ٱثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ ٱلْقَوْلُ وَمَنْ ءَامَنَ ۚ وَمَآ ءَامَنَ مَعَهُۥٓ إِلَّا قَلِيلٌ ٤٠
{40} "Mpaka ilipokuja amri yetu;" yaani, majaliwa yetu wakati wa wao kushukiwa na adhabu, "na tanuri ikafoka maji." Yaani, Mwenyezi Mungu aliiteremsha mbingu kwa maji ya kumiminika kwa wingi, na akaipasua ardhi yote kwa chemchemi, kiasi kwamba pia tanuru, ambazo ndiyo kwa kawaida ndipo pahali pa moto na pahali ambapo huwa mbali zaidi na maji, zikalipuka maji, na maji yakakutana kwa jambo lililokwisha pitishwa. "Tukamwambia" Nuhu: "Pakia humo katika kila kitu, jozi mbili ya dume na jike." Yaani, kutoka kwa kila aina ya viumbe, dume na jike ili asili ya sampuli zote za viumbe zibakie juu ya ardhi. Na ama sampuli zinginezo zinazozidi jozi, basi zitaangamia kwa sababu safina haiwezi kuzibeba. "Na ahali zako, isipokuwa wale ambao imekwisha wapitia hukumu;" yaani, wale waliokuwa makafiri, kama vile mtoto wake ambaye alizama. "Na watu walioamini." Na - hali ni kwamba - "hawakuamini pamoja naye isipokuwa wachache tu."