هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَـٰقَوْمِ لَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ ۚ وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ ۚ إِنَّهُم مُّلَـٰقُوا۟ رَبِّهِمْ وَلَـٰكِنِّىٓ أَرَىٰكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ ٢٩
{29} "Na enyi kaumu yangu! Mimi siwaombi juu ya haya" ya kuwalingania nyinyi "mali yoyote", ndiyo mkaona uzito wa gharama yake. "Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu." Na ni kama kwamba walimtaka awafukuze Waumini wanyonge, lakini akawaambia: "Na mimi sitawafukuza walioamini." Yaani, halinifailii wala haliendani na mimi; bali ninawapokea kwa moyo mkunjufu na ukarimu, na utukufu, na heshima. "Hakika wao watakutana na Mola wao Mlezi" na atawalipa kwa imani yao na uchamungu wao kwa Pepo za neema. "Lakini mimi nakuoneni mnafanya ujinga," kwa maana, mnaniamrisha niwafukuze vipenzi wa Mwenyezi Mungu na kuwaweka mbali nami, na kwa sababu mliikataa haki kwa kuwa walinifuata, na kwa kuwa mlitumia ushahidi wa kuonyesha ubatili wa haki kwa kauli yenu: Mimi ni binadamu mfano wenu, na kwamba hatuna ubora wowote juu yenu.