هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ يُعْرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ ٱلْأَشْهَـٰدُ هَـٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّـٰلِمِينَ ١٨
{18} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba hakuna yeyote “aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo?" Na anaingia katika hili kila mtu anayesema uongo juu ya Mwenyezi Mungu kwa kumnasibishia mshirika, au akamsifu kwa njia isiyoufailia utukufu Wake, au akajulisha juu Yake kwa yale ambayo hakuyasema, au akadai unabii au yasiyokuwa hayo miongoni mwa kumdanganyishia Mwenyezi Mungu. Basi hawa ndio watu madhalimu zaidi. "Hao wataletwa mbele ya Mola wao Mlezi" ili awalipe kwa dhuluma yao. Na atakapowahukumia adhabu kali, "mashahidi watasema;" yaani, wale waliowashuhudia kuzua kwao na uongo wao: "Hawa ndio waliomdanganyishia Mola wao Mlezi. Sikilizeni! Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate madhalimu." Yaani, laana isiyokoma. Kwa sababu, dhuluma yao imekwisha kuwa ni sifa yao isiyowaacha, na haiwezi kupunguzwa.