هود
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
الٓر ۚ كِتَـٰبٌ أُحْكِمَتْ ءَايَـٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ ١
{1} Yeye Mtukufu anasema: Hiki ni “Kitabu” kitukufu na uteremsho mtukufu, ambacho “Aya zake zimefanywa kuwa sawa sawa.” Yaani, zilifanywa kuwa kamilifu, nzuri, zenye habari za ukweli, zenye maamrisho na makatazo ya uadilifu, zenye maneno ya ufasaha na maana zake, "kisha zikapambanuliwa kwa kina." Yaani, zimepambanuliwa, na kubainishwa kunainisha kwa ya hali ya juu kabisa. "Kilichotoka kwa Mwenye Hekima" ambaye huviweka vitu pahali pake na kuviteremsha katika daraja zake. Haamrishi wala hakatazi isipokuwa kile ambacho hekima yake inataka. "Mwenye habari zote," anayajua ya dhahiri na ya ndani yote. Kwa hivyo, ikiwa kuzifanya kwake kuwa sawasawa, na kuzipambanua kwake kwa kina ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye hekima, Mwenye habari zote, basi usiulize baada ya haya kuhusu ukuu wake, utukufu wake, na kujumuisha kwa kwa hekima kamili na rehema pana.