يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِنَّ ٱلَّذِينَ حَقَّتْ عَلَيْهِمْ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ ٩٦ وَلَوْ جَآءَتْهُمْ كُلُّ ءَايَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُا۟ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ ٩٧
{96 - 97} Yeye Mtukufu Anasema, "Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwisha thibitika juu yao." Yaani, wao ni miongoni mwa wale waliopotea, walioangamia, watu wa Motoni, lazima wafikie yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwajalia na akawahukumia. Kwa hivyo, hawataamini hata kama itawajia kila ishara. Na ishara haziwazidishii isipokuwa kuvuka mipaka na upotofu ju ya upotofu wao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, bali walizidhulumu nafsi zao wenyewe kwa kuikataa kwao haki ilipowajia mara ya kwanza. Basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa kuziziba nyoyo zao, kusikia kwao na kuona kwao, ili wasiamini mpaka waione adhabu chungu waliyoahidiwa. Na hapo watajua kwa yakini kabisa kwamba waliyo juu yake ndiyo upotofu, na kwamba yale waliyowajia nayo Mitume ndiyo haki. Lakini yatakuwa katika wakati ambao imani yao haiwezi kuwafaidi kitu. Siku hiyo haitawafaa wale waliodhulumu udhuru wao, wala haitatakiwa toba yao. Ama ishara, hizo zinamfaa mwenye moyo au aliyetega sikio ilhali yupo anashuhudia.