يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوٓا۟ إِنَّ هَـٰذَا لَسِحْرٌ مُّبِينٌ ٧٦
{76} "Basi ilipowajia haki kutoka kwetu" ambayo ndiyo aina kubwa zaidi ya haki na tukufu yake zaidi. Nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye shingo zote zilimnyenyekea kwa sababu ya ukuu wake. Naye ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote, anayewalea viumbe wake wote kwa neema mbalimbali. Basi ilipowajia haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia mkono wa Musa, wakaikataa na hawakuikubali, na wakasema, "Hakika huu ni uchawi ulio dhahiri." Hawakutosheka - Mwenyezi Mungu awalaani - kupeana kwao mgongo wala kuikataa haki, mpaka walipoifanya kuwa batili ya batili zote, ambayo ni uchawi ambao uhakika wake ni kufichika na kugeuza jambo. Bali waliifanya kuwa uchawi ulio dhahiri, ilhali hiyo ndiyo haki iliyo dhahiri.