انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٧٤

ثُمَّ بَعَثْنَا مِنۢ بَعْدِهِۦ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَآءُوهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَمَا كَانُوا۟ لِيُؤْمِنُوا۟ بِمَا كَذَّبُوا۟ بِهِۦ مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ نَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلْمُعْتَدِينَ ٧٤

{74} Yaani, kisha baada ya Nuhu, amani iwe juu yake, tukawatuma "Mitume kwa kaumu zao" wanaokadhibisha, ili wawalinganie kwenye uwongofu, na wawaonye dhidi ya sababu za maangamizo, "wakawajia kwa Ishara zilizo wazi." Yaani, kila Nabii aliunga mkono ulinganizi wake kwa ishara zinazoonyesha usahihi wa kile alichokuja nacho. "Lakini hawakuwa wenye kuyaamini wale waliyoyakanusha kabla yake." Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaadhibu kwa maana alipowajia Mtume, wakaharakisha kumkadhibisha, kwa hivyo Mwenyezi Mungu akazifunga nyoyo zao na akawazuia kati yao na kuamini baada ya kwamba walikuwa wanaweza hilo. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, " Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao kama vile hawakuiamini mara ya kwanza." Na ndiyo maana akasema hapa: "Hivyo ndivyo tunavyoziziba nyoyo za wavukao mipaka." Yaani, tunaziziba, basi haziingiwi na heri yoyote. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walizidhulumu nafsi zao wenyewe kwa kukataa kwao haki ilipowajia na kule kukadhibisha kwao kwa mwanzo.