انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٧

هُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ لِتَسْكُنُوا۟ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ٦٧

{67} Na "Yeye ndiye aliyewajaalia usiku ili mtulie humo" kwa kulala usingizi na kutulia kwa sababu ya giza ambalo linafunika uso wa ardhi. Kwa maana, ikiwa mwanga ungeendelea, basi hawangeburudika wala kutulia. "Na" Mwenyezi Mungu aliufanya "mchana wa kuonea;" yaani, kuwa na mwangaza wanaona kwa huo viumbe, kwa hivyo wanaweza kuendesha maisha yao na masilahi ya dini yao na dunia yao. "Hakika katika haya zipo Ishara kwa kaumu wanaosikia," kutoka kwa Mwenyezi Mungu kusikia kwa kufahamu, na kukubali, na kutafuta mwelekeo, si kusikia kwa inda na ukaidi. Kwani katika hayo zipo ishara kwa kaumu wanaozisikia, ambao wanayatumia kama ushahidi kwamba Yeye pekee ndiye anayepaswa kuabudiwa, na kwamba Yeye ndiye Mungu wa haki, na kwamba uungu wa chochote kisichokuwa Yeye ni batili, na kwamba Yeye ndiye Mpole, Mwenye kurehemu, Mwenye kujua yote, Mwenye hekima.