يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ ءَامَنتُم بِهِۦٓ ۚ ءَآلْـَٔـٰنَ وَقَدْ كُنتُم بِهِۦ تَسْتَعْجِلُونَ ٥١
{51} “Tena je, ikishatokea ndiyo mtaiamini?” Basi hakika Imani hiyo haifai kitu wakati inapofika adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wataambiwa wakikaripiwa na kulaumiwa katika hali ile ambayo walidai kuwa wameamini: "Je, sasa?" Ndiyo mnaamini katika hali ya shida na mashaka, "Na ilhali mlikuwa mkiiharakishia?" Kwa maana desturi ya Mwenyezi Mungu katika waja wake ni kwamba anawaridhia wanapomwomba radhi kabla ya kutokea kwa adhabu. Lakini inapotokea adhabu, kuamini kwa nafsi hapo hakutainufaisha kitu, kama alivyosema Yeye kuhusu Firauni alipotaka kuzama. “Akasema, “Nimemini kuwa hakuna mungu isipokuwa yule waliyemwamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa Waislamu!" Basi huyo ataambiwa, “Je, sasa? Na ilhali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa waharibifu!" Na Mwenyezi Mungu Mtukufu alisema, “Lakini imani yao haikuwa yenye kuwanufaisha kitu wakati walipoiona adhabu yetu. Hii ndiyo desturi ya Mwenyezi Mungu ambayo alikwisha pitisha kwa waja wake." Na hapa akasema, "Tena je, ikishatokea ndio mtaiamini? Je, sasa?" mnadai kuamini, "Na ilhali mlikuwa mkiifanyia haraka?" Basi haya ndiyo mikono yenu iliyafanya, na haya ndiyo mliyoyafanyia haraka.