يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا ۚ إِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغْنِى مِنَ ٱلْحَقِّ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِمَا يَفْعَلُونَ ٣٦
{36} Basi jibu ni kwamba, hakika haya ni katika upambaji mambo wa Shetani kwa mwanadamu, na ni uongo mbaya zaidi na upotovu mkubwa zaidi mpaka akayaamini, na akayazoea, na akafikiri kuwa ndiyo haki ilhali si kitu. Na ndiyo maana akasema, “Na wala hawawafuati hao wanaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu washirika wake.” Yaani, hawawafuati kwa uhakika washirika wa Mwenyezi Mungu, kwa maana Mwenyezi Mungu kamwe hana mshirika yeyote, kiakili wala kimaandiko, bali wanafuata dhana tu. “Na hakika, dhana haifai kitu mbele ya haki.” Basi wakawaita kuwa ni miungu, na wakawaabudu pamoja na Mwenyezi Mungu. “Hayo si isipokuwa ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuteremsha uthibitisho wowote juu ya hayo.” "Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi yote wanayoyatenda,” na atawalipa kwa hayo kwa adhabu kali sana.