يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ ۚ قُلِ ٱللَّهُ يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ٣٤
{34} Yeye Mtukufu anasema akibainisha kutoweza kwa miungu ya washirikina na kutosifika kwayo na sifa zinazoweza kusababisha wachukuliwe kuwa miungu pamoja na Mwenyezi Mungu, “Sema: Je, yupo katika washirika wenu mwenye kuanzisha kuumba viumbe kisha akavirejesha?” Na huku ni kuuliza swali kwenye maana ya kukanusha na kuthibitisha. Yaani hakuna yeyote katika wao anayeanzisha kuumba viumbe kisha akavirudisha tena. Na ni dhaifu zaidi kuliko hivyo, na hawana uwezo hata zaidi yake. "Sema: Mwenyezi Mungu anaazisha kuumba viumbe, kisha anavirejesha” bila ya kuwa na mshirika yeyote wala msaidizi katika hayo. "Basi ni vipi mnadanganywa?” Yaani, mnageuzwa na mnaondolewa katika kumuabudu yule wa kipekee katika kuanzisha uumbaji na kuurudisha hadi katika kuwaabudu wale wasioumba chochote, nao wanaumbwa.