انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · يونس
السورة ١٠

يونس

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٧

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِـَٔايَـٰتِهِۦٓ ۚ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلْمُجْرِمُونَ ١٧

{17} Na “Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu na akazikadhibisha Ishara zake?” Na kama ningekuwa ni wa kukitunga, basi ningelikuwa dhalimu zaidi ya watu wote, na nikakosa kufaulu, na hali yangu isingefichika kwenu. Lakini niliwajia na Ishara za Mwenyezi Mungu, nanyi mkazikadhibisha, basi dhuluma ikathibiti kwenu hasa, na hakuna budi kwamba mambo yenu yatapotelea mbali, wala hamtapata kufaulu maadamu mtaendelea kuwa hivyo. Na kauli yake: "Wale wasiotaraji kukutana na Sisi husema...” hadi mwisho wa Aya iliashiria kuwa kilichowapeleka kwenye ukaidi huu ambao ulitoka kwao ni kutokuamini kwao kukutana na Mwenyezi Mungu na kutokuwa kwao na matumaini kwake, na kwamba mwenye kuamini kukutana na Mwenyezi Mungu, basi ni lazima afuate kitabu hiki na kukiamini, kwa sababu ana makusudio mazuri.