يونس
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلِ ٱنظُرُوا۟ مَاذَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَمَا تُغْنِى ٱلْـَٔايَـٰتُ وَٱلنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ ١٠١
{101} Yeye Mtukufu anawaita waja wake watazame vilivyo katika mbingu na ardhi, na kinachomaanishwa na hayo ni kutazama kwa kufikiri, na kuzingatia, na kutafakari yaliyo ndani yake, na yaliyojumuisha, na kutaka kubainishiwa. Kwani, katika hayo zipo Ishara kwa kaumu wanaoamini, na mazingatio kwa kaumu wenye yakini, zenye kuonyesha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye peke yake wa kuabudiwa, Msifiwa, Mwenye utukufu na ukarimu, na majina na sifa kuu. "Na Ishara zote na maonyo hayawafai kitu kaumu wasioamini." Kwa maana, wao hawafaidiki na ishara, kwa sababu ya kupeana kwao mgongo, na ukaidi wao.